Wednesday, March 28, 2018

Ajira Mpya 31 Halmashauri Ya Wilaya Ya Shinyanga Mjini

 Nafasi 31 za Kazi ya Mtendaji III Halmashauri ya Wilaya Shinyanga
Kumb No. SDC/C.4/7/4

Mkurugenzi Mtendaji Wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga anawatangazia wananchi wote wenye sifa kutuma maombi ya nafasi ya fani ya kazi ifuatayo kwa kuzingatia vigezo na maelekezo yaliyopo kwenye tangazo hili

MTENDAJI WA KIJIJI III NAFASI 31

(A)SIFA ZA MWOMBAJI

- Mwenye elimu ya kidato cha 4 na 6 na kuhitimu mafunzo ya Astashahada/Cheti katika moja ya fani zifuatazo
Utawala , Sheria, Elimu ya jamii usimamizi wa fedha maendeleo ya jamii na sayansi ya jamii kutoka chuo cha Serikali za mitaa Homboro Dodoma au chochote kinacho tamblika na serikali

(B)KAZI NA MAJUKUMU
- atakuwa Mtendaji na mshauri Mkuu wa Serikali ya Kijiji na kamati zake katika mipango ya maendeleo
- atakuwa afia mhasibu wa serikali ya kijiji na atasimamia mpato na matumizi ya Serikali ya kijiji
- atakuwa mlimzi wa amani na msimamizi wa utawala bora katika kijiji
- atatafsiri sera, utaratibu n kusimamia utekelezaji wa sheria ndogondogo za Halmashuri katika kijiji
- atakuwa katibu wa kamati wa halmashauri ya kijiji
- ataongoza vikao yvya maendeleo ya kijiji vitakavyowahususha wananchi na wataalam waliopo kwenye eneo lake

(C) MSHAHARA
kwa kuzingatia ngazi ya mishahara ya serikali yaani TGB

MASHARTI YA JUMLA
i. mwombaji awe na umri usiopungua miaka 18 - 45 (ambatanisha na cheti cha kuzaliwa)
ii. waombaji waambatanishe vivuli vya vyeti vyao vya elimu na taaluma pamoja na malelzo binafsi
iii. nakala zote za vyeti vya shule, chuo na cheti cha kualiwa vithibitishwe na mwanasheria au wakili yeyote aliyesajiliwa na kuthibitishwa
iv. katika brua ya maombi weka no yako ya simu inayopatikana wakati wote
v. barua zibandikwe picha 2 za passport size
vi. waombaji watakaokidhi vigezo watajulishwa tarehe ya uaili kwa kupitia namba za simu n anuani walizotumia kwenye barua zao za maombi ya kazi
vii. testimonials na provisional results havitakubaliwa
viii. mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 04/04/2018 saa 9: alasiri
ix. barua zitakazopelekwa kwa mkono hazitapokelewa

(D) JINSI YA KUTUMA MAOMBI
Barua zote ziandikwe kwa mkono wa mwombaji na kutumwa kwa njia ya posta kwa anuani ifuatayo

MKURUGENZI MTENDAJI,
HALMASHAURI YA WILAYA YA SHINYANGA,
S.L.P 113,
SHINYANGA.

Artikel Terkait