Wednesday, January 3, 2018

Nafasi 10 Za Ajira Kampuni Ya Expert Consultancy.

  Electricians x 5
Description

Kwa niaba ya mteja wetu mwenye kiwanda cha uzalishaji wa vyuma katika wilaya mkuranga tunahitaji mafundi umeme wa kufanya kazi za umeme kiwandani.

Majukumu ya Muombaji:
 Kufanya ufungaji, matengenezo na marekebisho ya vifaa vitumiavyo umeme kwa kuzingatia viwango vya usalama ipasavyo.
 Kutunza vitendea kazi, kupima vifaa vya umeme na kuhakikisha vipo salama muda wote;
 Kufunguwa na kutunza kadi za vitendea kazi vya umeme;
 Kufunga, kurekebisha na kusimamia mfumo wa uwekwaji umeme na vifaa vyake
 Kuchunguza na kutafuta makosa yanayopelekea mfumo wa umeme kutokufanya kazi
 Kuhakikisha udhaifu katika mfumo hautokei kwa kufanyia kazi makosa madogo madogo
 Kutengeneza michoro ya uwekaji nyaya, michoro ya itakavyokuwa na miongozo maususi ya kiufundi kwa ajili ya mfumo au marekebisho ya vifaa na mpangilio maalumu wa mtu anayeshughulikia uwekajia na marekebisho ya umeme.
 Kufanya uchunguzi wa mara kwa mara wa mfumo wa umeme, vifaa vya umeme na kutoa mapendekezo au kuweka utaratibu wa marekebisho au kubadilisha kifaa chenye tatizo.

Sifa za muombaji
 Awe na stashahada/cheti/vigezo vya VETA katika fani ya umeme
 Umri usiozidi miaka 45 tangu kuzaliwa.
 Ujuzi wa kutumia kompyuta ni sifa ya ziada.

 Mechanics x 5
Description

Kwa niaba ya mteja wetu mwenye kiwanda cha uzalishaji wa vyuma katika wilaya mkuranga tunahitaji mafundi Mekanika wa kufanya kazi za umeme kiwandani.

Majukumu ya Muombaji:
 Kusimamia usafi wa vitendea kazi/Vifaa na mathingira ya uzalishaji kiwandani;
 Kufanya maboresho na matengenezo ya machine za uzalishaji kiwandani.
 Kufanya ukaguzi wa kiufundi katika mitambo na vifaa vya uzalishaji kiwandani;
 Kufunguwa na kutunza kadi ya kumbukumbu ya shughuli za kila siku za mekanika;
 Kufuatilia utaratibu wa kazi kama utakavyopangwa na kiongozi wa idara;

Sifa za muombaji
 Awe na stashahada/cheti/vigezo vya VETA katika fani ya Mekanika
 Umri usiozidi miaka 45 tangu kuzaliwa.
 Ujuzi wa kutumia kompyuta ni sifa ya ziada.
 Lazima awe amefanya kazi katika viwanda vya chuma, Mabati au viwanda vinavyofanana na ivyo
 Awe na sifa nzuri kwa waajiri aliokwisha fanya nao kazi

Namna ya kutuma maombi:
Tuma wasifu wako (CV) tuu kwa barua pepe ifuatayo application@expertconsultancy.co.tz

Tuma maombi kabla ya tarehe 15/01/2018

Artikel Terkait